Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA- Dua ya Kumail ni moja ya dua adhimu na muhimu sana, inayopendelewa kusomwa kila siku ya Alkhamisi. Ni dua iliyojaa mafundisho ya kina kuhusu maombi, toba, na ukaribu na Mwenyezi Mungu, kama ilivyotufikia kupitia Amirul-Mu’minin Imam Ali (as).
Hawza ya Hazrat Zainab (sa) iliyoko Kigamboni, Dar-es-Salaam, ni chuo makhsusi kwa ajili ya kuwalea mabinti wa Kiislamu kielimu na kimaadili. Chuo hiki kipo chini ya usimamizi wa Jamiat Al-Mustafa (s) – Tanzania, na mbali na masomo ya kielimu yanayotolewa humo, wanafunzi pia hupatiwa malezi ya kiroho kwa kupitia mafundisho ya dua na ibada.
Katika harakati hizi, Dua Kumail inasomwa na kufundishwa kwa msisitizo maalumu, ikiambatana na kuelekezwa namna nzuri ya kuwasiliana na Mola kwa adabu, unyenyekevu, na maombi yaliyojaa maneno yenye maana na mapenzi, kama ilivyofundishwa na Ahlul-Bayt (as).
Kupitia utaratibu huu, wanafunzi wa chuo hiki wanalelewa kuwa waja wa kweli wa Mwenyezi Mungu, wanaojua thamani ya maombi na njia sahihi ya kumuomba Mola wao.
Your Comment